وَءَاخَرِينَ مِنۡهُمۡ لَمَّا يَلۡحَقُواْ بِهِمۡۚ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ
Na kwa wengine ambao bado hawajaungana nao. Na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Amemtuma yeye kwa watu wengine watakaokuja ambao bado hawajakuja miongoni mwa Waarabu na wengineo. Na Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, Peke Yake, Ndiye Mshindi mwenye kushinda juu ya kila kitu, Mwingi wa hekima katika maneno Yake na matendo Yake.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس