قَدۡ فَرَضَ ٱللَّهُ لَكُمۡ تَحِلَّةَ أَيۡمَٰنِكُمۡۚ وَٱللَّهُ مَوۡلَىٰكُمۡۖ وَهُوَ ٱلۡعَلِيمُ ٱلۡحَكِيمُ
Hakika Mwenyezi Mungu kakupeni Sharia ya kufungua viapo vyenu, na Mwenyezi Mungu ni Mola wenu. Na Yeye ni Mwenye kujua, Mwenye hikima.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Kwa hakika Amepasisha Mwenyezi Mungu kwenu, enyi Waumini, kuvihalalisha viapo vyenu kwa kuvitolea kafara. Kafara yenyewe ni kuwalisha masikini kumi au kuwavisha au kuacha shingo huru. Na asiyepata cha kutoa, basi afunge siku tatu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwanusuru nyinyi na kuyasimamia mambo yenu. Na Yeye Ndiye Mjuzi wa mambo yanayowafaa Akayapitisha kwenu, Ndiye Mwingi wa hekima kwenye maneno Yake na matendo Yake.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس