ﮪ
surah.translation
.
ﰡ
ﮫ
ﰀ
«Alif, Lām, Mīm» Yametangulia maelezo kuhusu herufi zilizokatwa- katwa na kutengwa mwanzo wa sura ya Al-Baqarah.
ﮭﮮ
ﰁ
Wafursi waliwashinda Warumi
katika sehemu za karibu za ardhi ya Shamu kuelekea Uajemi. Na Warumi watawashinda Wafursi
katika kipindi kisichopita miaka kumi na kisichopungua miaka mitatu. Ni ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka na kuwa juu, amri yote kabla ya ushindi wa Warumi na baada yake. Na siku hiyo ambayo Warumi watapata ushindi juu ya Wafursi Waumini wataifurahia nusura ya Mwenyezi Mungu kwa Warumi juu ya Wafursi.
Na Mwenyezi Mungu, Kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, Anamsaidia Anayemtaka na Anaacha kumsaidia Anayemtaka. Na Yeye Ndiye Mshindi Ambaye hakuna wa kushindana naye, Ndiye Mwenye kumrehemu Anayemtaka miongoni mwa viumbe Vyake. Na hilo lilithibitika, na Warumi waliwashinda Wafursi baada ya miaka saba, na Waislamu wakafurahi kwa hilo, kwa kuwa Warumi walikuwa ni watu wa Kitabu ingawa wamekipotosha.
Mwenyezi Mungu Amewaahidi Waumini, ahadi ya kukata isiyoenda kinyume, kuwapa ushindi Warumi juu ya Wafursi wenye kuabudu masanamu. Lakini wengi wa makafiri wa Makkah hawajui kwamba kile Alichokiahidi Mwenyezi Mungu ni kweli,
Wanayoyajua wao ni mambo yaliyofunuka wazi ya dunia na pambo lake, na wao kuhusu mambo ya Akhera na yale yanayowafaa huko wameghafilika, hawayafikirii.
Kwani hawakufikiri, hawa wakanushaji Mitume wa Mwenyezi Mungu na kukutana na Yeye, vile Mwenyezi Mungu Alivyowaumba, na kuwa wao Amewaumba na hawakuwa kitu chochote? Mwenyezi Mungu hakuumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake isipokuwa ni kwa ajili ya kusimamisha uadilifu, malipo mema na mateso na kutolea ushahidi upweke Wake na uweza Wake. Na kwa muda uliotajwa wa kukomea kwake nao ni Siku ya Kiyama. Na kwa hakika, wengi wa watu ni wenye kukataa na kukanusha kwa ujinga wao wa kutojua kuwa marejeo yao ni kwa Mwenyezi Mungu baada ya kutoweka kwao na kwa kughafilika kwao na Akhera.
Basi si waende hawa wanaomkanusha Mwenyezi Mungu, wanaoghafilika na Akhera, mwendo wa kufikiria na kuzingatia, wakapata kuona yalikuwa namna gani malipo ya ummah waliowakanusha Mitume wa Mwenyezi Mungu, kama vile kina ‘Ād na Thamūd? Hakika walikuwa wana nguvu zaidi kuliko wao kimiili na wana uwezo zaidi wa kustarehe na maisha, kwa kuwa waliilima ardhi na kuipanda mimea, na wakajenga majumba ya fahari na wakayakalia, hivyo basi waliuamirisha ulimwengu wao kuliko vile watu wa Makkah walivyouamirisha ulimwengu wao, na kusiwafalie kitu kule kuamirisha kwao wala urefu wa maisha yao. Na Mitume wao waliwajia na hoja waziwazi na dalili zenye kung’ara, wakawakanusha na Mwenyezi Mungu Akawaangamiza. Na Hakuwadhulumu kwa huko kuwaangamiza, isipokuwa wao wenyewe walijidhulumu wenyewe kwa kufanya ushirikina na kuasi.
Kisha ulikuwa mwisho wa waovu, miongoni mwa madhalimu na makafiri, ni mbaya zaidi na muovu zaidi, kwa kumkanusha kwao Mwenyezi Mungu na kuzifanyia shere aya Zake ambazo Aliziteremsha kwa Mitume Wake.
Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Ndiye Aliyepwekeka kwa kuanzisha uumbaji viumbe vyote. Na Yeye Ndiye Anayeweza, Peke Yake, kuvirudisha mara nyingine, kisha Kwake Yeye watarejea viumbe wote, Amlipe aliye mwema kwa wema wake na aliye mbaya kwa ubaya wake.
Na Siku ambayo Kiyama kitasimama wahalifu watakata tamaa ya kuokoka na adhabu, na utawapata wao mshangao utakaokata hoja zao.
Na washirikina , Siku hiyo, hawatokuwa na waombezi kati ya waungu wao waliokuwa wakiwaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, bali wao, hao waungu, watajiepusha nao na wao watajiepusha nao. Maombezi ni ya Mwenyezi Mungu Peke Yake, na hayatafutwi kutoka kwa mwingine.
Na Siku ambayo Kiyama kitasimama, watatengana watu wa Imani na watu wa ukafiri,
Ama waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, wenye kufanya matendo mema, watakuwa Peponi ambapo watakirimiwa, watafurahishwa na wataneemeshwa.
Na ama wale waliomkanusha Mwenyezi Mungu na wakayakanusha yale waliyokuja nayo Mitume na wakakanusha kufufuliwa baada ya kufa, basi hao watakaa adhabuni, ikiwa ni malipo ya kile walichokikanusha ulimwenguni.
Basi, enyi waumini, Mtakaseni Mwenyezi Mungu na mumuepushe na mshirika, mke na mtoto, na msifuni kwa sifa za ukamilifu kwa ndimi zenu, na mlithibitishe hilo kwa viungo vyenu vyote muingiliwapo na wakati wa jioni, na muingiliwapo na wakati wa asubuhi, na wakati wa usiku na wakati wa mchana.
Na ni Zake Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, shukrani na sifa njema katika mbingu na ardhi, na usiku na mchana.
Mwenyezi Mungu Anakitoa kilicho hai kutokana na kilichokufa, kama vile binadamu kutokana na tone la manii na ndege kutokana na yai, na Anakitoa kilichokufa kutokana na kilicho hai, kama vile tone la manii kutokana na binadamu na yai kutokana na ndege. Na Anahuisha ardhi kwa mimea baada ya kukauka na kuwa kavu. Na kwa namna hii ya kuhuisha mtatoka , enyi watu, makaburini mwenu mkiwa hai ili muhesabiwe na mulipwe.
Na miongoni mwa alama za Mwenyezi Mungu zinazoonyesha ukubwa wake na ukamilifu wa uweza Wake, ni kuwa Alimuumba baba yenu Ādam kutokana na mchanga, kisha nyinyi binadamu mnaenea kwenye ardhi kwa kuzaliana mnatafuta fadhila za Mwenyezi Mungu.
Na miongoni mwa alama zenye kuonyesha ukubwa Wake na ukamilifu wa uweza wake ni kuwa Amewaumba wake kwa ajili yenu kutokana na jinsi yenu, enyi wanaume, ili nafsi zenu zijitulize kwao na ziburudike, na Akatia mapenzi na huruma baina ya mwanamke na mumewe. Hakika katika uumbaji huo wa Mwenyezi Mungu pana alama zenye kuonyesha uweza wa Mwenyezi Mungu na kupwekeka Kwake kwa watu wenye kufikiria na kuzingatia.
Na miongoni mwa dalili za uweza wa Mwenyezi Mungu ni uumbaji mbingu na kuwa juu kwake bila ya nguzo, na uumbaji ardhi ikiwa imekunjuka na kupanuka, na kutafautiana lugha zenu na kuwa mbalimbali rangi zenu. Hakika katika hayo kuna mazingatio kwa kila mwenye elimu na busara.
Na miongoni mwa dalili za uweza huu ni kuwa Mwenyezi Mungu Amewawekea usingizi uwe ni mapumziko kwenu ya usiku au mchana, kwani katika kulala yanapatikana mapumziko na kuondokewa na machovu, na Amewawekea mchana ambapo ndani yake mnaenda huku na kule kutafuta riziki. Hakika katika hayo kuna dalili ya ukamilifu wa uweza wa Mwenyezi Mungu na upitishaji matakwa Yake kwa watu wanaosikia mawaidha usikiaji wa kutia akilini, kufikiria na kuzingatia.
Na miongoni mwa dalili za uweza Wake, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake ni kuwaonyesha umeme, mkaogopa vimondo na mkawa na matumaini ya mvua, na Anateremsha mvua kutoka mawinguni ikahuisha ardhi baada ya kuwa katika hali ya ukame na ukavu. Hakika katika hayo kuna dalili ya ukamilifu wa uweza wa Mwenyezi Mungu na ukubwa wa hekima Yake na wema Wake kwa kila Mwenye akili ya kujiongoza.
Na miongoni mwa alama Zake zenye kuonyesha uweza Wake ni kuwa mbingu na ardhi zinasimama, zinatulia na zinajikita kwa Amri Yake, zisitikisike na mbingu isianguke juu ya ya ardhi, kisha Mwenyezi Mungu Atakapowaita nyinyi kwenye kufufuliwa Siku ya Kiyama, muda si muda mtajikuta mnatoka makaburini kwa haraka.
Ni wa Mwenyezi Mungu, Peke Yake, wote waliyoko mbinguni na ardhini, miongoni mwa Malaika, binadamu, majini, wanyama, mimea na visivyo na uhai, wote hao wanafuata amri Yake wanaunyenyekea ukamilifu Wake.
Na ni Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Anayeanzisha uumbaji viumbe kutoka kwenye hali ya kutokuwako, kisha Atawarudisha wakiwa hai baada ya kufa. Na kuwarudishia viumbe uhai baada ya kufa ni rahisi kwa Mwenyezi Mungu kuliko kuanzisha kuwaumba, na yote mawili ni rahisi Kwake. Na ni ya Mwenyezi Mungu sifa ya hali ya juu katika kila anachosifiwa, Hakuna chochote mfano Wake, na Yeye Ndiye Mwenye kusikia, Ndiye Mwenye kuona, Na Yeye Ndiye Mshindi Asiyeshindwa, Ndiye Mwingi wa hekima katika maneno Yake na vitendo Vyake na uendeshaji mambo ya viumbe Vyake.
Mwenyezi Mungu Amewapigia mfano, enyi washirikina, utokao na nafsi zenu: Je kuna yoyote, kati ya watumwa wenu na wajakazi wenu, anayeshirikiana na nyinyi katika riziki yenu na mkaona kuwa nyinyi na wao muko sawa katika hiyo, ikawa mnawaogopa wao kama mnavyowaogopa waungwana washirika katika ugawaji wa mali zenu? Nyinyi hamtaridhika na hilo, basi vipi mtaridhika na hilo upande wa Mwenyezi Mungu kwa kumfanya kuwa Ana mshirika miongoni mwa viumbe Vyake? Kwa mfano wa ufafanuzi huu, tunawafafanulia ushahidi na hoja watu wenye akili timamu ambao watanufaika nao.
Bali washirikina walifuata matamanio yao kwa kuwaiga wazazi wao bila ujuzi wowote, wakashirikiana nao katika ujinga na upotevu. Na hakuna yoyote anayeweza kumuongoza yule ambaye Mwenyezi Mungu Amempoteza kwa sababu ya kuendelea kwake kwenye ukafiri na ukaidi. Na hawa hawana wasaidizi wa kuwaokoa na adhabu ya Mwenyezi Mungu.
Basi simamisha uso wako, ewe Mtume, wewe na waliokufuata na uendelee kwenye msimamo wa dini ambayo Mwenyezi Mungu Amekuwekea, nayo ni Uislamu ambao Mwenyezi Mungu Ameifanya ilingane na maumbile ya watu. Basi kuendelea kwenu kubaki kwenye Uislamu, na kushikamana kwenu nao ni kushikamana na umbile la Mwenyezi Mungu la kumuamini Mwenyezi Mungu Peke Yake. Hapana ugeuzaji wa uumbaji wa Mwenyezi Mungu na Dini Yake, kwani hiyo ndiyo njia iliyonyoka yenye kupelekea kwenye radhi za Mwenyezi Mungu, Mola wa viumbe wote, na Pepo Yake. Lakini wengi wa watu hawajui kuwa yale niliyokumrisha nayo, ewe Mtume, ndiyo Dini ya haki na si nyigine.
Na muwe ni wenye kurejea kwa Mwenyezi mungu kwa kutubia na kumtakasia matendo mema. Na muogopeni Yeye kwa kufanya maamrisho na kujiepusha na makatazo, na msimamishe Swala kikamilifu kwa nguzo zake na mambo yake yanayopasa na sharti zake, na msiwe ni miongoni mwa wenye kumshirikisha mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu katika ibada.
Na msiwe ni miongoni mwa washirikina na watu wa (kufuata) matamanio na mambo ya uzushi, walioibadilisha dini yao na wakaigeuza kwa kuchukuwa baadhi yake na kuacha baadhi yake kwa kufuata matamanio yao, wakawa ni makundi na mapote, wanafuata mikao ya viongozi wao na vyama vyao na maoni yao, wanasaidiana wao kwa wao katika batili, kila watu wa kundi wanashangilia na kufurahia mkao wao, wanajihukumia wenyewe kuwa wao wako kwenye haki na wasiokuwa wao wako kwenye ubatilifu.
Na yakiwapata watu matatizo na misukosuko wanamuomba Mola wao, hali ya kumtakasia, Awaondolee mashaka, na Anapowarehemu na Akawaondolea mashaka, punde si punde linatoka pote la watu kati yao wakarudi kwenye ushirikina mara nyingine wakamuabudu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu.
Ili wakanushe kile tulichowapa na kuwaneemesha kwacho cha kutatuliwa matatizo na kuondolewa shida. Basi stareheni, enyi washirikina, kwa neema na ukunjufu katika dunia hii, mtakijua mtakachokikuta cha adhabu na mateso.
Au tuliwateremshia hawa washirikina hoja yenye kutoa mwangaza na kitabu kisicho na shaka kitamke kueleza usahihi wa ushirikina wao na ukanushaji wao Mwenyezi Mungu na aya Zake?
Na tunapowaonjesha watu neema itokayo kwetu ya afya, uzima na mafanikio, wanafurahia hilo furaha ya kiburi na majivuno, na sio furaha ya shukrani. Na yakiwapata wao magonjwa, umasikini, kuogopa na dhiki kwa sababu ya dhambi zao na maasia yao, ghafula wao wanakata tamaa kuwa hayo yatawaondokea. Na hii ni tabia ya wengi wa watu katika hali ya neema na matatizo.
Kwani hawajui kwamba Mwenyezi Mungu Anamkunjulia riziki Anayemtaka kwa kumjaribu: atashukuru au atakufuru? Na (kwani hawajui kwamba Yeye) Anambania riziki Anayemtaka kwa kumjaribu: je atavumilia au atababaika? Hakika katika kukunjulia na kubania kuna alama (za utendakazi wa Mwenyezi Mungu) kwa watu wanaomuamini Mwenyezi Mungu na wanaojua hekima ya Mwenyezi Mungu na rehema Yake.
Basi mpe , ewe mwenye kuamini, jamaa yako wa karibu haki yake ya kuunga kizazi na sadaka na mambo mengine ya wema. Na mpe masikini na mwenye uhitaji aliyekatikiwa na njia (kwa kuishiwa na pesa akiwa safarini) Zaka na sadaka. Kwani kutoa huko ni bora kwa wale wanaoukusudia kupata radhi ya Mwenyezi Mungu kwa matendo yao mema. Na wanaofanya matendo haya na megineyo miongoni mwa matendo mema, wao ndio wenye kufaulu kupata malipo ya Mwenyezi Mungu, ndio wenye kuokoka na mateso Yake.
Na mkopo wowote wa pesa mnaoutoa kwa makusudio ya riba, na kutaka kuzidisha mkopo huo ili kupatikane ongezeko katika mali ya watu, basi mbele ya Mwenyezi Mungu hayaongezeki, bali Anayaondolea baraka na kuyabatilisha. Na Zaka na sadaka mnazotoa kuwapatia wastahiki kwa kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu na kutaka malipo yake, basi hiki ndicho ambacho Mwenyezi Mungu Anakikubali na Atawaongezea mara nyingi zaidi.
Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Ndiye Aliyewaumba nyinyi, enyi watu, kisha Akawapa riziki katika uhai huu, kisha Atawafisha muda wenu ukomapo, kisha Atawafufua kutoka makaburini mkiwa muko hai mpate kuhesabiwa na kulipwa. Je kuna yoyote miongoni mwa washirika wenu anayefanya chochote katika hayo? Ameepukana Mwenyezi Mungu na Ametakasika na ushirikina wa hawa wenye kumshirikisha.
Uharibifuumejitokezabaranina baharini, kama vile ukame, uchache wa mvua, wingi wa magonjwa na majanga, kwa sababu ya maasia yanayofanywa na binadamu, hivyo basi Awapatie adhabu kwa baadhi ya matendo waliyoyatenda ulimwenguni wapate kutubia kwa Mwenyezi Mungu, kutakasika na sifa na upungufu ni Kwake, na warudi nyuma waache maasia na matendo yao yatengenezeke na mambo yao yalingane sawa.
Sema, ewe Mtume, kuwaambia wenye kuyakanusha uliyokuja nayo, «Tembeeni kwenye sehemu za ardhi matembezi ya kuzingatia na kutia mambo akilini, na mtazame vile ulivyokuwa mwisho wa ummah waliopita wenye kukanusha, kama vile watu wa Nūḥ, ‘Ād na Thamūd, mtakuta kwamba mwisho wao walioishia ulikuwa mbaya zaidi na kikomo hiko walichokomea kilikuwa kibaya zaidi, kwani wengi wao walikuwa ni wenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu.
Basi elekeza uso wako, ewe Mtume, upande wa Dini iliyonyoka, nayo ni Uislamu, hali ya kutekeleza maamrisho yake na kujiepusha makatazo yake. Na ushikamane nayo kabla Siku ya Kiyama haijaja, kwani ijapo Siku hiyo, ambayo hakuna anayeweza kuirudisha, viumbe watapambanuka wakiwa makundi- makundi yalio tafauti ili waoneshwe matendo yao.
Mwenye kukanusha basi mateso ya ukanushaji wake yatamshukia yeye, nayo ni kukaa milele Motoni. Na mwenye kuamini na akafanya matendo mema basi hao wanajitayarishia wenyewe makao ya Peponi, kwa sababu ya kushikamana kwao na utiifu wa Mola wao.
Hivyo basi Mwenyezi Mungu Awalipe wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wakafanya matendo mema kwa fadhila Zake na wema Wake, hakika Yeye Hawapendi wakanushaji kwa kuwa Ana hasira na ghadhabu juu yao.
Na miongoni mwa alama za Mwenyezi Mungu zenye kuonyesha kuwa Yeye ndiye Mungu wa kweli Peke Yake, Asiye na Mshirika, na kuwa Ana uweza mkubwa, ni kule kutuma upepo mbele ya mvua ukiwa ni wenye kuleta habari njema, kwa kuyasukuma mawingu, hapo nafsi zikaingiwa na furaha kwa hilo, ili awaonjeshe rehema Yake kwa kuwateremshia mvua ambayo kwayo miji inahuika na pia waja, na ili jahazi zitembee baharini kwa amri Yake na matakwa Yake, na ili mtafute fadhila Zake kwa kufanya biashara na megineyo. Mwenyezi Mungu Amefanya hayo yote ili mzishukuru neema Zake na mmuabudu Yeye Peke Yake.
Kwa hakika tuliwatuma kabla yako wewe, ewe Mtume, Mitume waende kwa watu wao kwa kubashiria na kuonya, wawaite kwenye upwekeshaji (wa Mwenyezi Mungu) na wawatahadharishe na ushirikina. Wakawajia na miujiza na hoja zenye mwangaza, na wengi wao wakamkanusha Mola wao, na kwa hivyo tukawatesa wale waliotenda mabaya miongoni mwao, tukawaangamiza na tukawapa ushindi wafuasi wa Mitume. Na hivyo ndivyo tunavyowafanya wenye kukukanusha wanapoendelea kukukanusha na wasiamini.
Mwenyezi Mungu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Ndiye Anayetuma upepo ukayasukuma mawingu yaliyojaa maji, na Mwenyezi Mungu Akayasambaza mbinguni vile Anavyotaka, Akayafanya ni vipande vilivyotenganika mbalimbali, hapo ukaiona mvua inatoka mawinguni. Na Aipelekapo Mwenyezi Mungu kwa waja wake, ghafla utawakuta wameingiwa na bashasha na wanafurahi kwa kuwa Mwenyezi Mungu Amewaletea hiyo.
Na ingawa wao kabla ya kuteremka mvua walikuwa katika hali ya kukata tamaa na kutokuwa na matumaini kwa sababu ya kutonyeshewa na mvua.
Basi Tazama, ewe mwenye kuangalia, mtazamo wa kutia akilini na kuzingatia, athari za mvua kwenye mimea, nafaka na miti, ujionee vipi Mwenyezi Mungu Anaipa uhai ardhi baada ya kuwa imekufa, Akaiotesha mimea na nyasi? Hakika Yule aliyeweza kuihuisha ardhi hii Ndiye Atakayehuisha wafu, na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza, hakuna kinachomshinda.
Na tukiupeleka kwenye mashamba yao ya nafaka na mimea yao upepo wenye kuharibu, wakaiona mimea yao imeharibika kwa upepo huo, ikawa imekuwa rangi ya manjano baada ya kuwa rangi ya kijani, wangalikaa baada ya kuiona wakimkufuru Mwenyezi Mungu na kuzikanusha neema Zake.
Kwa hakika wewe, ewe Mtume, humsikilizishi yule ambaye moyo wake umekufa au mashikio yake yamezibana yakawa hayaisikii haki. Basi usibabaike wala usisikitike kwa kukataa kukuamini hawa washirikina, kwani wao ni kama viziwi na wafu, hawasikii wala hawahisi hata kama wako mbele yako, basi itakuwa vipi iwapo hawako na wewe na wamekupa mgongo.
Na hukuwa wewe, ewe mtume, ni mwenye kumuongoza yule aliyefanywa kipofu na Mwenyezi Mungu asiione njia ya uongofu. Utakayemsikilizisha akanufaika kwa kusikia si mwingine isipokuwa yule anayeziamini aya zetu, basi hao ni wenye kuandama na kufuata amri ya Mwenyezi Mungu.
Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Ndiye Ambaye Amewaumba kwa maji ya udhaifu na unyonge, nayo ni tone la manii, kisha akaleta, baada ya udhaifu wa utoto, nguvu za utu uzima, kisha akaleta, baada ya nguvu hizi, udhaifu wa uzee na ukongwe. Anaumba Anachotaka cha udhaifu na nguvu. Na Yeye Ndiye Mjuzi wa viumbe Vyake, Ndiye Muweza wa kila kitu.
Na siku kitakapokuja Kiyama na Atakapo Mwenyezi Mungu kuwafufua viumbe kutoka makaburini mwao, wataapa washirikina kwamba hawakukaa duniani isipokuwa kipindi kifupi cha wakati. Watasema urongo katika kiapo chao kama walivyokuwa wakisema urongo duniani na wakiikataa haki ambayo Mitume walikuja nayo.
Na watasema wale waliopewa elimu na imani ya Mwenyezi Mungu, miongoni mwa Malaika, Mitume na Waumini, «Mlikuwa mmekaa katika kile Alichokiandika Mwenyezi Mungu, kutokana na ujuzi Wake uliotangulia, kuanzia siku mliyoumbwa mpaka mkafufuliwa. Basi hii ndio Siku ya Ufufuzi, lakini nyinyi mlikuwa hamjui, ndipo mkaikataa duniani na mkaikanusha.»
Basi Siku ya Kiyama, hazitawafaa madhalimu nyudhuru zao wazitowazo, na hawatatakiwa wamridhishe Mwenyezi Mungu kwa kutubia na kutii, isipokuwa watateswa kwa makosa yao na maasia yao.
Hakika tuliwafafanulia watu, katika hii Qur’ani, kila mfano ili kuwasimamishia hoja na kuthibitisha kuwa Mwenyezi Mungu ni Mmoja, Aliyetukuka na kuwa juu. Na lau ungaliwajia na hoja yoyote yenye kuonyesha ukweli wako, wale waliokukanusha wangalisema kukwambia, «Hamkuwa nyinyi, ewe Mtume na wafuasi wako, isipokuwa ni warongo katika yale mambo mnayotuletea.»
Mfano wa muhuri huu, Mwenyezi Mungu Anapiga muhuri juu ya nyoyo za wasioujua uhakika wa kile unachowaletea, ewe Mtume, kutoka kwa Mwenyezi Mungu kutokana na mazingatio haya na miujiza iliyo waziwazi.
Basi vumilia, ewe Mtume, kwa yale yanayokupata ya makero ya watu wako kwako na kukukanusha kwao, kwani ahadi ya Mwenyezi Mungu kwako ya ushindi, uthabiti na malipo mema ni kweli isiyo na shaka. Na wasikubabaishe wakakuweka kando na Dini yako wale wasiokuwa na yakini ya Agizo (la Siku ya Kiyama) na wasioamini kufufuliwa na malipo.