ﯿ
surah.translation
.
ﰡ
Pindi mbingu zitakapopasuka na ukaharibika mpango wake.
Na pindi nyota zitakapoangukiana.
Na pindi Mwenyezi Mungu Atakapozifanya bahari kulipuka na maji yake kutoweka.
Na pindi makaburi yatakapogeuzwa kwa kufufuliwa waliokuwamo ndani yake.
Wakati huo itajua kila nafsi vitendo vyake vyote ilivyovifanya, vilivyotangulia na vilivyoahirika na italipwa kwa vitendo hivyo.
Ewe binadamu unayekanusha kufufuliwa! Ni kipi kilichokufanya uhadaike na ughurike kuhusu Mola wako Mpaji Mwenye kheri nyingi, Anayestahiki kushukuriwa na kutiiwa?
Kwani si Yeye Aliyekuumba, Akalisawazisha umbo lako, Akakuweka katika hali ya sawa na Akakurekibisha ili uweze kutekeleza nyadhifa zako,
katika sura yoyote ile Aliyoitaka Akakuumba?
Mambo hayako kama vile mnavyosema kwamba nyinyi mna haki ya kumuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Bali nyinyi mnaikanusha Siku ya Hesabu na Malipo.
Na mjue kuwa wako na nyinyi Malaika wachunguzi,
ﮃﮄ
ﰊ
watukufu kwa Mwenyezi Mungu, waandishi wa yale waliyowakilishwa kuyadhibiti. Hakiwapiti, katika vitendo vyenu na siri zenu, chochote.
Wanayajua mnayoyafanya, ya kheri au ya shari.
Hakika wachamungu wanaotekeleza haki za Mwenyezi Mungu na haki za waja wake watakuwa kwenye neema.
Hakika watu waovu waliopuuza haki za Mwenyezi Mungu na haki za waja wake watakuwa katika Moto mkali.
Ukali wake, Moto huo, utawapata Siku ya Malipo.Na wala wao hawatakuwa ni wenye kughibu,
wakawa hawamo ndani ya Moto wa Jahanamu, si kwa kutoka wala kwa kufa.
Ni kipi kinachokujuza ni upi utukufu wa Siku ya Hesabu?
Kisha ni kipi kinachokujuza ni upi utukufu wa Siku ya Hesabu?
Siku ya Hesabu, hataweza yoyote kumnufaisha yoyote. Na amri zote Siku Hiyo ni za Mwenyezi Mungu Peke yake Ambaye hakuna mwenye kumshinda, wala hakuna mwenye kumtendesha nguvu, wala hakuna mwenye kushindana na Yeye.