ﯬ
surah.translation
.
ﰡ
Wanapohudhuria wanafiki kwenye kikao chako, ewe Mtume, husema kwa ndimi zao, «Tunakubali kuwa wewe kwa kweli ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu Anajua kuwa wewe ni mtume wa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu Anashuhudia kwamba wanafiki ni warongo katika ushahidi wao kwako walioudhihirisha na wakauapia kwa ndimi zao na huku wameuficha ukanushaji wao kwake.
Ukweli ni kwamba wanafiki wamevifanya viapo vyao wanavyoviapa ni kinga na ngao ya kuwakinga wasihukumiwe na kuadhibiwa, na wamejizuia wenyewe na kuwazuia watu njia ya mwenyezi Mungu iliyonyoka. Kwa kweli wao, ni maovu mno yale ambayo walikuwa wakiyafanya,
kwa kuwa wao wameamini kijuujuu kisha kindanindani wamekufuru. Ndipo Mwenyezi Mungu Akapiga muhuri juu ya nyoyo zao kwa ukafiri wao, Hivyo basi wao hawayaelewi yale yenye maslahi kwao.
Na unapowatazama wanafiki hawa, yanakufurahisha maumbile yao na mandhari yao, na wanapozungumza unayasikiliza mazungumzo yao kwa ufasaha wa ndimi zao, na hali wao kutokamana na utupu wa nyoyo zao kuwa hazina Imani na akili zao kuwa hazina fahamu wala elimu yenye manufaa, ni kama vigogo vilivyotegemezwa kwenye ukuta, visivyokuwa na uhai.wanadhania kila sauti ya ukelele inawashukia wao na ina madhara kwao kwa kujua kwao uhakika wa hali yao na uoga wao mwingi na hofu iliyojikita nyoyoni mwao. Wao ndio maadui wa kikwelikweli wenye uadui mwingi kwako wewe na kwa Waumini. Basi jichunge na wao, Mwenyezi Mungu Amewadhalilisha wao na Amewatoa kwenye rehema Yake. Basi ni vipi wao wanaiepuka haki na wanaelekea kwenye yale ambayo wao wamo ndani yake ya unafiki na upotevu.
Na wanapoambiwa hawa wanafiki, «Njooni huku hali ya kutubia mtake udhuru wa hayo yaliyotokea kwenu ya maneno maovu na mazungumzo ya ufidhuli, ili Mtume wa Mwenyezi Mungu awaombee Mwenyezi Mungu msamaha wa dhambi zenu , huvigeuza vichwa vyao na wakavitikisa kwa njia ya shere na kiburi. Na utawaona, ewe Mtume, wanakupa mgongo na huku wao wanalifanyia kiburi jambo la kufuata yale ambayo walitakiwa wayafuate.
Yanalingana kwa wanafiki hawa, uwaombee msamaha kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ewe Mtume, au usiwaombee, kwani Mwenyezi Mungu Hatazisamehe dhambi zao kabisa kwa sababu ya kuendelea kwao na uasi na kujikita kwao kwenye ukafiri. Hakika Mwenyezi Mungu Hawaelekezi kwenye Imani watu wanaomkanusha waliotoka nje ya utiifu Kwake.
Wanafiki hawa ndio wao wanaosema kuwaambia watu wa Madina, «Msitoe kuwasaidia Maswahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu waliohama mpaka wajiepushe naye.» Ni za Mwenyezi Mungu, Peke Yake, hazina za mbinguni na ardhini na vilivyomo humo miongoni mwa riziki, Humpa Anayemtaka na Humnyima Anayemtaka, lakini wanafiki hawaelewi kwamba riziki inatoka kwa Mwenyezi Mungu kwa ujinga wao wa kutomjua Yeye, kutakasika na kila upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake.
Wanasema hawa wanafiki, «Tutakaporudi Madina, kundi letu lenye nguvu zaidi litalitoa kundi la Waumini lililo twevu zaidi.» Kwa hakika, nguvu na ushindi ni vya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, ni vya Mtume Wake, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na ni vya wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, si vya wale wasiokuwa wao, lakini wanafiki hawalijui hilo kwa ujinga wao uliokita mizizi.
Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkazifuata Sheria Zake kivitendo! Yasiwashughulishe nyinyi mali yenu wala wana wenu na kumuabudu Mwenyezi Mungu na kumtii. Na yoyote atakayeshughulishwa na mali Yake na watoto Wake na hilo la kumuabudu Mwenyezi Mungu, basi hao ndio waliopunjwa hisa zao za makaribisho ya Mwenyezi Mungu na rehema Yake.
Na toeni, enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, sehemu ya kile tulichowapa katika njia za kheri, mkilikimbilia hilo kabla ya kifo hakijamjia mmoja wenu na kuziona dalili zake na alama zake, na hapo aseme kwa kujuta, «Mola wangu! Si unipe muda na uahirishe kifo changu kipindi kifupi! Nipate kutoa sadaka sehemu ya mali yangu na niwe miongoni mwa watu wema wachamungu.»
Na wala Mwenyezi Mungu hatoichelewesha nafsi yoyote utakapokuja wakati wa kifo chake na umri wake ukakoma. Na Mwenyezi Mungu, kutakasika na kila sifa ya upungufu ni Kwake, ni mtambuzi wa yale mnayoyatenda: mema na mabaya, na Awetawalipa nyinyi kwa hayo.