ترجمة سورة قريش

الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
ترجمة معاني سورة قريش باللغة السواحلية من كتاب الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس .

Oneni ajabu ya mazowea ya Makureshi, amani walionayo, kuwaendea uzuri mambo yao,
kupangika na kusahilika misafara yao ya kwenda Yamani kipindi cha kusi na kwenda Shamu kipindi cha kaskazi, ili kuleta vitu wanavyohitajia.
Basi, wamshukuru na kumuabudu Bwana wa Nyumba hii ya Alkaba, Ambaye kwa ajili Yake wametukuzwa, na wampwekeshe na kumtakasia ibada.
Ambaye Amewapa wao chakula wakati wa njaa kali na akawapa amani na utulivu kutokana na kicho kikubwa na babaiko.
Icon