إِذۡ هَمَّت طَّآئِفَتَانِ مِنكُمۡ أَن تَفۡشَلَا وَٱللَّهُ وَلِيُّهُمَاۗ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلۡيَتَوَكَّلِ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ ١٢٢
Al-Imran 3:122
سورة آل عمران
Madina
Aya: 122/200
Ukurasa 66
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Makundi mawili miongoni mwenu yakaingiwa na woga kuwa watashindwa - na hali Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi wao; na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Kumbuka, ewe Mtume, yale mambo yaliyowahusu kina Banū Salimah na Banū Ḥārithah wakati walipowaza kurudi nyuma, wao na kiongozi wao, mnafiki Abdullāh bin Ubayy bin Salūl, kwa kuogopa kukutana na adui. Lakini Mwenyezi Mungu Aliwalinda na Akawahifadhi wakaenda pamoja na wewe wakimtegemea Mwenyezi Mungu. Na kwa Mwenyezi Mungu, Peke Yake, na wajitegemeze Waumini.
Al-Imran 3:122
Inapakia kisomo…
0:00