وَمَا كَانَ قَوۡلَهُمۡ إِلَّآ أَن قَالُواْ رَبَّنَا ٱغۡفِرۡ لَنَا ذُنُوبَنَا وَإِسۡرَافَنَا فِيٓ أَمۡرِنَا وَثَبِّتۡ أَقۡدَامَنَا وَٱنصُرۡنَا عَلَى ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡكَٰفِرِينَ ١٤٧
Al-Imran 3:147
سورة آل عمران
Madina
Aya: 147/200
Ukurasa 68
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Wala kauli yao haikuwa ila ni kusema: Mola wetu Mlezi! Tughufirie madhambi yetu na kupita kwetu kiasi katika mambo yetu, na isimamishe imara miguu yetu na utunusuru tuwashinde kaumu ya makafiri. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Na halikuwa neno la hawa wenye kusubiri isipokuwa ni kusema, «Ewe Mola wetu! Tusamehe madhambi yetu na yaliyotokea kwetu ya kuruka mipaka katika mambo ya dini yetu na uzithibitishe nyayo zetu, tusipate kukimbia tunapopigana na adui yetu na utunusuru na yule anayepinga umoja wako na unabii wa Manabii wako.
Al-Imran 3:147
Inapakia kisomo…
0:00