فَمَن يُرِدِ ٱللَّهُ أَن يَهۡدِيَهُۥ يَشۡرَحۡ صَدۡرَهُۥ لِلۡإِسۡلَٰمِۖ وَمَن يُرِدۡ أَن يُضِلَّهُۥ يَجۡعَلۡ صَدۡرَهُۥ ضَيِّقًا حَرَجࣰا كَأَنَّمَا يَصَّعَّدُ فِي ٱلسَّمَآءِۚ كَذَٰلِكَ يَجۡعَلُ ٱللَّهُ ٱلرِّجۡسَ عَلَى ٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ ١٢٥
Al-An'am 6:125
سورة الأنعام
Makka
Aya: 125/165
Ukurasa 144
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Basi yule ambaye Mwenyezi Mungu anataka kumhidi humfungulia kifua chake kwa Uislamu. Na anaye taka apotee hukifanya kifua chake kina dhiki, kimebana, kama kwamba anapanda mbinguni. Namna hivi Mwenyezi Mungu anajaalia uchafu juu ya wasio amini. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Basi yule ambaye Mwenyezi Mungu Anataka kumuafukia aikubali haki, Anakikunjua kifua chake kukubali Imani na upweke wa Mwenyezi Mungu; na yule ambaye Anataka kumpoteza , Anakifanya kifua chake kiwe katika hali ya dhiki kubwa na kukunjika katika kuukubali uongofu, kama hali ya anayepaa kwenye tabaka za anga za juu, hapo akapatwa na uzito mkubwa wa kuvuta pumzi. Na kama anavyovifanya Mwenyezi Mungu vifua vya makafiri vibanike sana na kukunjika, hivyo basi ndivyo Atakavyowapatia adhabu wale wasiomuamini.
Al-An'am 6:125
Inapakia kisomo…
0:00