قُلۡ إِنَّنِي هَدَىٰنِي رَبِّيٓ إِلَىٰ صِرَٰطࣲ مُّسۡتَقِيمࣲ دِينࣰا قِيَمࣰا مِّلَّةَ إِبۡرَٰهِيمَ حَنِيفࣰاۚ وَمَا كَانَ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ ١٦١
Al-An'am 6:161
سورة الأنعام
Makka
Aya: 161/165
Ukurasa 150
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Sema: Kwa hakika mimi Mola wangu Mlezi ameniongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka, Dini iliyo sawa kabisa, ambayo ndiyo mila ya Ibrahim aliye kuwa mwongofu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina, «Mimi Ameniongoza Mola wangu kwenye njia iliyolingana sawa yenye kufikisha kwenye Pepo Yake, nayo ni Dini ya Uislamu yenye kusimamia mambo ya dunia na ya Akhera; nayo ni Dini ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu, Dini ya Ibrāhīm, amani imshukiye. Na Ibrāhīm, amani imshukiye, hakuwa ni miongoni mwa wenye kumshirikisha pamoja na Mwenyezi Mungu asiyekuwa Yeye.»
Al-An'am 6:161
Inapakia kisomo…
0:00