وَهُوَ ٱلَّذِي جَعَلَكُمۡ خَلَٰٓئِفَ ٱلۡأَرۡضِ وَرَفَعَ بَعۡضَكُمۡ فَوۡقَ بَعۡضࣲ دَرَجَٰتࣲ لِّيَبۡلُوَكُمۡ فِي مَآ ءَاتَىٰكُمۡۗ إِنَّ رَبَّكَ سَرِيعُ ٱلۡعِقَابِ وَإِنَّهُۥ لَغَفُورࣱ رَّحِيمُۢ ١٦٥
Al-An'am 6:165
سورة الأنعام
Makka
Aya: 165/165
Ukurasa 150
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Naye ndiye aliye kufanyeni makhalifa wa duniani, na amewanyanyua baadhi yenu juu ya wengine daraja kubwa kubwa, ili akujaribuni kwa hayo aliyo kupeni. Hakika Mola Mlezi wako ni Mwepesi wa kuadhibu, na hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Na Mwenyezi Mungu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Ndiye Aliyewafanya nyinyi mushike nafasi za waliowatangulia katika ardhi baada ya Mwenyezi Mungu kuwaondoa na kuwaweka nyinyi badala yao, mupate kuiamirisha baada yao kwa kumtii Mola wenu. Na amewainua daraja baadhi yenu, katika mapato na nguvu, juu ya wengine ili kuwapa mtihani katika alichowapa miongoni mwa neema Zake, apate kuwa wazi kwa watu mwenye kushukuru na asiyeshukuru. Hakika Mola wako ni Mwepesi wa adhabu kwa aliyemkanusha na kumuasi. Na Yeye ni Mwingi wa msamaha kwa aliyemuamini na akafaya matendo mema na akatubia na dhambi yenye kuangamiza, ni Mwenye huruma Kwake. Al-Ghafūr (Mwingi wa kusamehe)na Al-Raḥīm (Mwenye kurehemu) ni majina mawili matukufu katika majina ya Mwenyezi Mungu.
Al-An'am 6:165
Inapakia kisomo…
0:00