وَمَا مِن دَآبَّةࣲ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَا طَٰٓئِرࣲ يَطِيرُ بِجَنَاحَيۡهِ إِلَّآ أُمَمٌ أَمۡثَالُكُمۚ مَّا فَرَّطۡنَا فِي ٱلۡكِتَٰبِ مِن شَيۡءࣲۚ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّهِمۡ يُحۡشَرُونَ ٣٨
Al-An'am 6:38
سورة الأنعام
Makka
Aya: 38/165
Ukurasa 132
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na hapana mnyama katika ardhi, wala ndege anaye ruka kwa mbawa zake mbili, ila ni umma kama nyinyi. Hatukupuuza Kitabuni kitu chochote. Kisha kwa Mola wao Mlezi watakusanywa. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Hakuna katika ardhi mnyama yoyote anayetembea chini au ndege anayepaa juu kwa mbawa zake isipokuwa ni aina ya makundi yaliyoumbwa kama nyinyi. Hatukuacha katika Allawh, Almaḥfūd (Ubao Uliohifadhiwa) chochote isiopokuwa tumekithibitisha. Kisha wao, Siku ya Kiyama, watafufuliwa wapelekwe kwa Mola wao, na hapo Mwenyezi Mungu Atamhesabu kila mtu kwa alilolitenda.
Al-An'am 6:38
Inapakia kisomo…
0:00