وَهُوَ ٱلَّذِيٓ أَنشَأَكُم مِّن نَّفۡسࣲ وَٰحِدَةࣲ فَمُسۡتَقَرࣱّ وَمُسۡتَوۡدَعࣱۗ قَدۡ فَصَّلۡنَا ٱلۡأٓيَٰتِ لِقَوۡمࣲ يَفۡقَهُونَ ٩٨
Al-An'am 6:98
سورة الأنعام
Makka
Aya: 98/165
Ukurasa 140
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na Yeye ndiye aliye kuzalisheni kutokana na nafsi moja. Pako pahali pa kutulia na pa kupita njia. Hakika tumezichambua Ishara hizi kwa watu wanao fahamu. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Na Mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, Ndiye Aliyeanza kuwaumba, enyi watu, kutokana na Ādam, amani imshukiye, Alipomuumba kwa udongo, kisha mkawa nyinyi ni kizazi chenye kuendelea kutokana na yeye, Akawafanyia kituo cha nyinyi kutulia, nacho ni zao za wanawake; na Akawafanyia hazina ya nyinyi kuhifadhiwa , nayo ni migongo ya wanaume. Tumeshawabainishia hoja na kuwapambanulia dalili na kuzithibitisha kwa watu wenye kufahamu vituo vya hoja na sehemu za mazingatio.
Al-An'am 6:98
Inapakia kisomo…
0:00