۞ فَـَٔامَنَ لَهُۥ لُوطࣱۘ وَقَالَ إِنِّي مُهَاجِرٌ إِلَىٰ رَبِّيٓۖ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ ٢٦
Al-'Ankabut 29:26
سورة العنكبوت
Makka
Aya: 26/69
Ukurasa 399
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Lut'i akamuamini, na akasema: Mimi nahamia kwa Mola wangu Mlezi. Hakika Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Lūṭ akamuamini Ibrāhīm na akaufuata mwenendo wake. Na Ibrāhīm akasema, «Mimi nitaiwacha nchi ya watu wangu na nitaenda kwenye ardhi iliyobarikiwa, nayo ni Shām, kwani Mwenyezi Mungu ni Mshindi Asiyeshindwa ni Mwingi wa hekima katika uendeshaji mambo Wake.
Al-'Ankabut 29:26
Inapakia kisomo…
0:00