وَمَآ أَرۡسَلۡنَا فِي قَرۡيَةࣲ مِّن نَّبِيٍّ إِلَّآ أَخَذۡنَآ أَهۡلَهَا بِٱلۡبَأۡسَآءِ وَٱلضَّرَّآءِ لَعَلَّهُمۡ يَضَّرَّعُونَ ٩٤
Al-A'raf 7:94
سورة الأعراف
Makka
Aya: 94/206
Ukurasa 162
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na hatukumtuma Nabii yeyote katika mji ila tuliwapatiliza wakaazi wake kwa taabu na mashaka ili wapate kunyenyekea. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Na hatukumtuma Nabii kwenye kijiji chochote kuwalingania watu wake kumuabudu Mwenyezi Mungu na kuwakataza ushirikina ambao wanao, kisha wakamkanusha, isipokuwa tuliwapa mtihani wa shida na mikasa, tukawatia kwenye miili yao magonjwa na ndwele, na katika mali yao ufukara na uhitaji, kwa matumaini kwamba wanyenyekee, waelekee kwa Mwenyezi mungu na warudi kwenye haki.
Al-A'raf 7:94
Inapakia kisomo…
0:00