ثُمَّ بَدَّلۡنَا مَكَانَ ٱلسَّيِّئَةِ ٱلۡحَسَنَةَ حَتَّىٰ عَفَواْ وَّقَالُواْ قَدۡ مَسَّ ءَابَآءَنَا ٱلضَّرَّآءُ وَٱلسَّرَّآءُ فَأَخَذۡنَٰهُم بَغۡتَةࣰ وَهُمۡ لَا يَشۡعُرُونَ ٩٥
Al-A'raf 7:95
سورة الأعراف
Makka
Aya: 95/206
Ukurasa 162
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Kisha Sisi hubadilisha mahala pa ubaya kwa wema, hata wakazidi, na wakasema: Taabu na raha ziliwafikia baba zetu. Basi kwa ghafla tukawashika, hali ya kuwa hawajatambua. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Kisha tukaigeuza hali nzuri ya mwanzo mahali pa hali mbaya, wakawa wana afya katika miili yao, na ukunjufu na neema katika mali zao, ili kuwapa muhula, kwani wakashukuru. Hayo yote hayakuwa na faida kwao, na hawakuzingatia wala hawakukomeka na ushirikina waliokuwa nao na wakasema, «Hii ndiyo hali ya ulimwengu kwa watu wake, kuna siku njema na siku mbaya; na hayo ndiyo yaliyowapitia baba zetu hapo nyuma.» Basi, punde si punde, tuliwashika kwa adhabu wakiwa wametulia, hawakuwa wakifikiria kuwa wataangamizwa.
Al-A'raf 7:95
Inapakia kisomo…
0:00