وَلَنَبۡلُوَنَّكُم بِشَيۡءࣲ مِّنَ ٱلۡخَوۡفِ وَٱلۡجُوعِ وَنَقۡصࣲ مِّنَ ٱلۡأَمۡوَٰلِ وَٱلۡأَنفُسِ وَٱلثَّمَرَٰتِۗ وَبَشِّرِ ٱلصَّٰبِرِينَ ١٥٥
Al-Baqarah 2:155
سورة البقرة
Madina
Aya: 155/286
Ukurasa 24
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Hapana shaka tutakujaribuni kwa chembe ya khofu, na njaa, na upungufu wa mali na watu na matunda. Na wabashirie wanao subiri, -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Tutawapa, tena tutawapa, mtihani wa kitu hafifu cha hali ya kuogopa, njaa, upungufu wa mali, iwe ni uzito kuyapata au yaondoke, upungufu wa watu: kwa kufa au kufa-shahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu, na kwa upungufu wa matunda ya mitende na mizabibu na nafaka: kwa kupungua mazao yake au kuharibika kwake.Wape, ewe Nabii, habari njema, wale wenye subira juu ya haya na mfano wake, kwa yale yatakayowafurahisha na kuwapendeza ya mwisho mwema duniani na Akhera.
Al-Baqarah 2:155
Inapakia kisomo…
0:00