كُتِبَ عَلَيۡكُمُ ٱلۡقِتَالُ وَهُوَ كُرۡهࣱ لَّكُمۡۖ وَعَسَىٰٓ أَن تَكۡرَهُواْ شَيۡـࣰٔا وَهُوَ خَيۡرࣱ لَّكُمۡۖ وَعَسَىٰٓ أَن تُحِبُّواْ شَيۡـࣰٔا وَهُوَ شَرࣱّ لَّكُمۡۚ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ وَأَنتُمۡ لَا تَعۡلَمُونَ ٢١٦
Al-Baqarah 2:216
سورة البقرة
Madina
Aya: 216/286
Ukurasa 34
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Mmeandikiwa kupigana vita, navyo vinachusha kwenu. Lakini huenda mkachukia kitu nacho ni kheri kwenu. Na huenda mkapenda kitu nacho ni shari kwenu. Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Mwenyezi Mungu Amewafaradhia, enyi Waumini, kupigana na Makafiri, hali ya kuwa ni jambo lenye kuchukiwa na nyinyi kimaumbile, kwa uzito wake na hatari zake nyingi. Na huenda mkakichukia kitu nacho, kwa uhakika wake, ni kheri kwenu. Na huenda mkakipenda kitu kwa ajili ya raha na ladha za karibu zilizomo, nacho, kwa uhakika wake, ni shari kwenu. Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Analijua lenye kheri kwenu, na nyinyi hamlijui hilo. Kwa hivyo harakisheni kupigana jihadi katika njia Yake.
Al-Baqarah 2:216
Inapakia kisomo…
0:00