مَّن ذَا ٱلَّذِي يُقۡرِضُ ٱللَّهَ قَرۡضًا حَسَنࣰا فَيُضَٰعِفَهُۥ لَهُۥٓ أَضۡعَافࣰا كَثِيرَةࣰۚ وَٱللَّهُ يَقۡبِضُ وَيَبۡصُۜطُ وَإِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ ٢٤٥
Al-Baqarah 2:245
سورة البقرة
Madina
Aya: 245/286
Ukurasa 39
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Ni nani atakaye mkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mwema ili amzidishie mzidisho mwingi, na Mwenyezi Mungu hukunja na hukunjua. Na Kwake Yeye mtarejea. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Ni yupi ambaye atatoa katika njia ya Mwenyezi Mungu, kutoa kuliko kuzuri kwa kutarajia malipo, Mwenyezi Mungu Apate kumuongezea nyongeza nyingi zisizohesabika za thawabu na malipo mema? Hakika Mwenyezi Mungu Anazuia na Anatoa. Kwa hivyo, toeni wala msijali, kwani Yeye Ndiye Mruzuku, Anambana Anayemtaka, miongoni mwa waja Wake, katika riziki na Anaikunjua, hiyo riziki, kwa wengine. Ana hekima kubwa katika hayo. Na Kwake Yeye Peke Yake mtarudi baada ya kufa, na hapo Atawalipa kwa vitendo vyenu.
Al-Baqarah 2:245
Inapakia kisomo…
0:00