إِن تُبۡدُواْ ٱلصَّدَقَٰتِ فَنِعِمَّا هِيَۖ وَإِن تُخۡفُوهَا وَتُؤۡتُوهَا ٱلۡفُقَرَآءَ فَهُوَ خَيۡرࣱ لَّكُمۡۚ وَيُكَفِّرُ عَنكُم مِّن سَيِّـَٔاتِكُمۡۗ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ خَبِيرࣱ ٢٧١
Al-Baqarah 2:271
سورة البقرة
Madina
Aya: 271/286
Ukurasa 46
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Mkizidhihirisha sadaka ni vizuri; na mkizificha mkawapa mafakiri kwa siri basi hivyo ni kheri kwenu, na yatakuondoleeni baadhi ya maovu yenu. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Mkizidhihirisha zile mnazozitoa sadaka kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ni sadaka nzuri mliyoitoa. Na mkizitoa kwa siri mkawapa mafukara, ni bora zaidi kwenu kwa kuwa hivyo ni mbali na ria. Na katika utoaji sadaka pamoja na ikhlasi kuna kusamehewa madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu Anayajua mambo ya ndani; hakuna kinachofichika Kwake katika mambo yenu na Atamlipa kila mtu kwa amali yake.
Al-Baqarah 2:271
Inapakia kisomo…
0:00