ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ وَمَا بَيۡنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامࣲ ثُمَّ ٱسۡتَوَىٰ عَلَى ٱلۡعَرۡشِۖ ٱلرَّحۡمَٰنُ فَسۡـَٔلۡ بِهِۦ خَبِيرࣰا ٥٩
Al-Furqan 25:59
سورة الفرقان
Makka
Aya: 59/77
Ukurasa 365
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Ambaye ameziumba mbingu na ardhi, na viliomo ndani yake kwa siku sita. Kisha akatawala juu ya A'rshi, Arrahman, Mwingi wa Rehema! Uliza khabari zake kwa wamjuaye. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Aliyeumba mbingu na ardhi na vilivyoko baina yake kwa Siku sita, kisha akalingana juu ya '“Arsh - yaani Akawa juu na Akaangatika- kulingana kunakonasibiana na utisho Wake, Yeye Ndiye Mwingi wa rehema. Basi muulize, ewe Mtume, Mtambuzi kuhusu Yeye. Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika, Anajikusudia Mwenyewe Aliyetukuka, kwani Yeye Ndiye Anayejua sifa Zake, ukuu Wake na utukufu Wake. Na hakuna yoyote, katika binadamu, anayemjua zaidi Mwenyezi Mungu wala anayetambua habari Zake zaidi kuliko mja Wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye.
Al-Furqan 25:59
Inapakia kisomo…
0:00