لَا يُقَٰتِلُونَكُمۡ جَمِيعًا إِلَّا فِي قُرࣰى مُّحَصَّنَةٍ أَوۡ مِن وَرَآءِ جُدُرِۭۚ بَأۡسُهُم بَيۡنَهُمۡ شَدِيدࣱۚ تَحۡسَبُهُمۡ جَمِيعࣰا وَقُلُوبُهُمۡ شَتَّىٰۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ قَوۡمࣱ لَّا يَعۡقِلُونَ ١٤
Al-Hashr 59:14
سورة الحشر
Madina
Aya: 14/24
Ukurasa 547
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Hawatapigana nanyi kwa mkusanyiko isipo kuwa katika vijiji vilivyo zatitiwa kwa ngome, au nyuma ya kuta. Wao kwa wao vita vyao ni vikali. Utawadhania kuwa wako pamoja, kumbe nyoyo zao ni mbali mbali. Hayo ni kwa kuwa wao ni watu wasio na akili. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Hawatakabiliana na nyinyi Mayahudi wakiwa wamejikusanya isipokuwa wakiwa kwenye miji iliyohifadhiwa kwa ngome na mahandaki, au nyuma ya kuta ambazo wanazitumia kwa kujificha kwa uoga wao na kicho kilichojikita ndani ya nyoyo zao. Uadui wao baina yao ni mkubwa, utadhani kuwa wao wamekusanyika kwenye neno moja, lakini nyoyo zao ziko mbalimbali, na hiyo ni kwa sababu wao ni watu wasioitia akilini amri ya Mwenyezi Mungu wala kuzizingatia aya Zake.
Al-Hashr 59:14
Inapakia kisomo…
0:00