وَمَنۡ أَرَادَ ٱلۡأٓخِرَةَ وَسَعَىٰ لَهَا سَعۡيَهَا وَهُوَ مُؤۡمِنࣱ فَأُوْلَٰٓئِكَ كَانَ سَعۡيُهُم مَّشۡكُورࣰا ١٩
Al-Isra 17:19
سورة الإسراء
Makka
Aya: 19/111
Ukurasa 284
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na anaye itaka Akhera, na akazifanyia juhudi a'mali zake, naye ni Muumini, basi hao juhudi yao itakuwa ni ya kushukuriwa. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Na yoyote aliyekusudia kwa matendo yake mema kupata malipo ya Nyumba ya Akhera yenye kusalia na akajishughulisha nayo kwa kumtii Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na hali yeye ni mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na kuamini thawabu Zake na malipo Yake makubwa, basi hao matendo yao ni yenye kukubaliwa ni yenye kuhifadhiwa kwa ajili yao mbele ya Mola wao na watapata malipo yake.
Al-Isra 17:19
Inapakia kisomo…
0:00