۞ وَلَقَدۡ كَرَّمۡنَا بَنِيٓ ءَادَمَ وَحَمَلۡنَٰهُمۡ فِي ٱلۡبَرِّ وَٱلۡبَحۡرِ وَرَزَقۡنَٰهُم مِّنَ ٱلطَّيِّبَٰتِ وَفَضَّلۡنَٰهُمۡ عَلَىٰ كَثِيرࣲ مِّمَّنۡ خَلَقۡنَا تَفۡضِيلࣰا ٧٠
Al-Isra 17:70
سورة الإسراء
Makka
Aya: 70/111
Ukurasa 289
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na hakika tumewatukuza wanaadamu, na tumewapa vya kupanda nchi kavu na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa tulio waumba. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Kwa hakika tumewatukuza watu wa kizazi cha Ādam kwa akili na kuwapelekea Mitume, na tukawadhalilishia vilivyoko ulimwenguni vyote: tukawadhalilishia wanyama barani wa kuwapanda na vyombo baharini vya kuwabeba, tukawaruzuku vilaji na vinywaji vizuri na tukawapa daraja kubwa juu ya viumbe wengi.
Al-Isra 17:70
Inapakia kisomo…
0:00