وَأَنَّهُۥ كَانَ رِجَالࣱ مِّنَ ٱلۡإِنسِ يَعُوذُونَ بِرِجَالࣲ مِّنَ ٱلۡجِنِّ فَزَادُوهُمۡ رَهَقࣰا ٦
Al-Jinn 72:6
سورة الجن
Makka
Aya: 6/28
Ukurasa 572
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na hakika walikuwako wanaume katika watu walio kuwa wakitafuta kujikinga kwa wanaume wa kijini; kwa hivyo wakawazidisha madhambi. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
«Na kwamba wanaume miongoni mwa binadamu walikuwa wakijilinda na wanaume miongoni mwa majini, na hawa wanaume wa kijini wakawazidi binadamu kwa kuwa binadamu wanajilinda nao kwa hofu, kicho na kutishika.» Kujilinda huku na asiyekuwa Mwenyezi Mungu, ambako Mwenyezi Munghu Aliwatangazia watu wa zama za watu wa ujinga, ni katika ushirikina mkubwa ambao Mwenyezi Mungu hausamehe isipokuwa kwa kutubia kidhati kutokana nao. Katika aya hii pana onyo kali juu ya kitendo cha kuwaewndea wachawi, makuhani na mfano wao.
Al-Jinn 72:6
Inapakia kisomo…
0:00