ٱلَّذِينَ ضَلَّ سَعۡيُهُمۡ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَهُمۡ يَحۡسَبُونَ أَنَّهُمۡ يُحۡسِنُونَ صُنۡعًا ١٠٤
Al-Kahf 18:104
سورة الكهف
Makka
Aya: 104/110
Ukurasa 304
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Ni wale ambao juhudi yao katika maisha ya dunia imepotea bure, nao wanadhani kwamba wanafanya kazi nzuri. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Wao ni wale ambao matendo yao yalipotea katika maisha ya ulimwengu- nao ni washirikina wa watu wako na wengineo kati ya wale waliopotea njia ya sawa wasiwe kwenye uongofu wala usawa- na hali wao wanadhania kuwa wanayatengeneza matendo yao.
Al-Kahf 18:104
Inapakia kisomo…
0:00