إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَٱلَّذِينَ هَادُواْ وَٱلصَّٰبِـُٔونَ وَٱلنَّصَٰرَىٰ مَنۡ ءَامَنَ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ وَعَمِلَ صَٰلِحࣰا فَلَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ ٦٩
Al-Ma'idah 5:69
سورة المائدة
Madina
Aya: 69/120
Ukurasa 119
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Hakika walio amini, na Mayahudi na Masabii na Wakristo, walio muamini Mwenyezi Mungu, na Siku ya mwisho, na wakatenda mema, basi hawatakuwa na khofu wala hawatahuzunika. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Hakika wale walioamini (nao ni Waislamu), Mayahudi na al- Ṣābiūn (Masabai, nao ni watu waliosalia kwenye umbile lao na hawana dini fulani waifuatayo), Wanaswara (nao ni wafuasi wa al-Masīḥ), waliomuamini Mwenyezi Mungu miongono mwao Imani kamilifu, nayo ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu, kumuamini Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na yale aliyokuja nayo, wakaiyamini Siku ya Mwisho na wakatenda matendo mema, basi hao hawatakuwa na hofu yoyote juu ya janga la Siku ya Kiyama wala wao hawatakuwa na huzuni juu ya yale waliyoyaacha nyuma yao duniani.
Al-Ma'idah 5:69
Inapakia kisomo…
0:00