لَقَدۡ أَخَذۡنَا مِيثَٰقَ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ وَأَرۡسَلۡنَآ إِلَيۡهِمۡ رُسُلࣰاۖ كُلَّمَا جَآءَهُمۡ رَسُولُۢ بِمَا لَا تَهۡوَىٰٓ أَنفُسُهُمۡ فَرِيقࣰا كَذَّبُواْ وَفَرِيقࣰا يَقۡتُلُونَ ٧٠
Al-Ma'idah 5:70
سورة المائدة
Madina
Aya: 70/120
Ukurasa 119
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Tulifanya agano na Wana wa Israili, na tukawatumia Mitume. Kila alipo wajia Mtume kwa wasio yapenda nafsi zao wengine waliwakanusha na wengine wakawauwa. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Kwa hakika tulichukuwa ahadi ya mkazo kwa Wana wa Isrāīl katika Taurati kuwa watasikia na watatii na tukawapelekea kwa ahadi hiyo Mitume wetu. Lakini walivunja ile ahadi iliyochukuliwa kwao, wakafuata matamanio yao na wakawa kila akiwajia Mtume, miongoni mwa hao Mitume, kwa yale ambayo nafsi zao haziyataki, wanamfanyia uadui: wakawakanusha baadhi yao na wakawaua wengine.
Al-Ma'idah 5:70
Inapakia kisomo…
0:00