إِنَّ ٱلَّذِينَ يُحَآدُّونَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ كُبِتُواْ كَمَا كُبِتَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۚ وَقَدۡ أَنزَلۡنَآ ءَايَٰتِۭ بَيِّنَٰتࣲۚ وَلِلۡكَٰفِرِينَ عَذَابࣱ مُّهِينࣱ ٥
Al-Mujadilah 58:5
سورة المجادلة
Madina
Aya: 5/22
Ukurasa 542
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Hakika wanao pinzana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake, watadhalilishwa kama walivyo dhalilishwa wale walio kuwa kabla yao. Na tulikwisha teremsha Ishara zilizo wazi. Na makafiri watapata adhabu ya kufedhehesha. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Hakika ya wale wanaomfanyia uadui na Mwenyezi mungu na Mtume Wake na wakaenda kinyume na amri zao, watadhalilishwa na watatwezwa kama walivyodhalilishwa ummah waliokuwa kabla yao waliopingana na Mwenyezi Mungu na Mitume Wake. Na tumeteremsha aya zenye hoja zilizo wazi zinazoonyesha kuwa Sheria ya Mwenyezi Mungu na mipaka Yake ni kweli. Na wenye kuzikanusha aya hizo watapata adhabu yenye kudhalilisha ndani ya moto wa Jahanamu.
Al-Mujadilah 58:5
Inapakia kisomo…
0:00