لَن تَنفَعَكُمۡ أَرۡحَامُكُمۡ وَلَآ أَوۡلَٰدُكُمۡۚ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ يَفۡصِلُ بَيۡنَكُمۡۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرࣱ ٣
Al-Mumtahinah 60:3
سورة الممتحنة
Madina
Aya: 3/13
Ukurasa 549
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Hawatakufaeni jamaa zenu, wala watoto wenu Siku ya Kiyama. Mwenyezi Mungu atapambanua baina yenu, na Mwenyezi Mungu anayaona mnayo yatenda. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Hawatawanufaisha nyinyi jamaa zenu wa karibu wala watoto wenu kitu chochote mnapofanya urafiki na wakanushaji kwa ajili yao. Siku ya Kiyama Mwenyezi Mungu Atawatenganisha nyinyi na wao, Awatie Peponi wanaomtii na Awatie Motoni wanaomuasi. Na Mwenyezi Mungu Anayaona mnayoyafanya, hakuna chochote kinachofichamana Kwake cha maneno yenu na matendo yenu.
Al-Mumtahinah 60:3
Inapakia kisomo…
0:00