وَمَآ أَنزَلۡنَا عَلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَ إِلَّا لِتُبَيِّنَ لَهُمُ ٱلَّذِي ٱخۡتَلَفُواْ فِيهِ وَهُدࣰى وَرَحۡمَةࣰ لِّقَوۡمࣲ يُؤۡمِنُونَ ٦٤
An-Nahl 16:64
سورة النحل
Makka
Aya: 64/128
Ukurasa 273
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na hatukukuteremshia Kitabu isipo kuwa uwabainishie yale ambayo wanakhitalifiana, na kiwe Uwongofu na Rehema kwa watu wanao amini. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Na hatukukuteremshia Qur’ani, ewe Mtume, isipokuwa ni uwafunulie watu wazi yale ambayo walikuwa wakitafautiana juu yake, ya dini na hukumu, ili hoja zisimame kwao kwa maelezo yako ambayo hayauachii upotofu njia ya kuingia nyoyoni. Na kwa kuwa Qur’ani ni uongofu, haitoi nafasi ya kutunduwaa, nayo ni rehema kwa Waumini katika kufuata kwao uongofu na kujiepusha kwao na upotevu.
An-Nahl 16:64
Inapakia kisomo…
0:00