وَمِن ثَمَرَٰتِ ٱلنَّخِيلِ وَٱلۡأَعۡنَٰبِ تَتَّخِذُونَ مِنۡهُ سَكَرࣰا وَرِزۡقًا حَسَنًاۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةࣰ لِّقَوۡمࣲ يَعۡقِلُونَ ٦٧
An-Nahl 16:67
سورة النحل
Makka
Aya: 67/128
Ukurasa 274
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na kutokana na matunda ya mitende na mizabibu mnatengeneza ulevi na riziki nzuri. Hakika katika hayo ipo Ishara kwa wanao tumia akili. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Na miongoni mwa neema zetu kwenu ni yale matunda ya mitende na mizabibu mnayoyachukuwa mkayatengeneza pombe yenye kulewesha - na hii na kabla haijaharamishwa- na chakula kizuri. Hakika katika hayo yaliyotajwa pana ushahidi juu ya uweza wa Mwenyezi Mungu kwa watu wenye kuzitia akilini hoja hizo wakazizingatia.
An-Nahl 16:67
Inapakia kisomo…
0:00