وَيَوۡمَ نَبۡعَثُ فِي كُلِّ أُمَّةࣲ شَهِيدًا عَلَيۡهِم مِّنۡ أَنفُسِهِمۡۖ وَجِئۡنَا بِكَ شَهِيدًا عَلَىٰ هَٰٓؤُلَآءِۚ وَنَزَّلۡنَا عَلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَ تِبۡيَٰنࣰا لِّكُلِّ شَيۡءࣲ وَهُدࣰى وَرَحۡمَةࣰ وَبُشۡرَىٰ لِلۡمُسۡلِمِينَ ٨٩
An-Nahl 16:89
سورة النحل
Makka
Aya: 89/128
Ukurasa 277
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na (waonye) siku tutakapo wainua mashahidi katika kila umma wakiwashuhudia kwa yanayo tokana na wao, na tutakuleta wewe uwe shahidi juu ya hao. Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinacho bainisha kila kitu, na ni uwongofu, na rehema, na bishara kwa Waislamu. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Na kumbuka, ewe Mtume, pindi tutakapomleta, Siku ya Kiyama, katika kila ummah miongoni mwa ummah zote, shahidi juu yao: naye ni Mtume ambaye Mwenyezi Mungu Alimpeleka kwao anayetokana na wao wenyewe na kwa lugha yao, na tukakuleta wewe, ewe Mtume, ukiwa ni shahidi juu ya ummah wako. Na kwa kweli, tumekuteremshia Qur’ani ikiwa na ufafanuzi wa kila jambo linalohitajia maelezo, kama hukumu za halali na haramu, malipo mema na mateso na yasiyokuwa hayo, na ili iwe ni uongofu wenye kutoa kwenye upotevu, na ni rehema kwa atakayeiamini na kuifuata kivitendo, na iwe ni bishara njema kwa Waumini kwamba watakuwa na mwisho mwema.
An-Nahl 16:89
Inapakia kisomo…
0:00