قَالُواْ ٱطَّيَّرۡنَا بِكَ وَبِمَن مَّعَكَۚ قَالَ طَٰٓئِرُكُمۡ عِندَ ٱللَّهِۖ بَلۡ أَنتُمۡ قَوۡمࣱ تُفۡتَنُونَ ٤٧
An-Naml 27:47
سورة النمل
Makka
Aya: 47/93
Ukurasa 381
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Wakasema: Tuna kisirani nawe na wale walio pamoja nawe. Yeye akasema: Uaguzi wa ukorofi wenu uko kwa Mwenyezi Mungu; lakini nyinyi ni watu mnao jaribiwa. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Wakasema watu wa Ṣāliḥ kumwambia, «Tumepata ukorofi kwa sababu yako wewe na watu walioko na wewe kati ya wale walioingia katika dini yako.» Ṣāliḥ aliwaambia, «Wema Anaowapatia Mwenyezi Mungu au uovu, basi hua umekadiriwa kwenu na Mwenyezi Mungu na Atawapa malipo yake. Bali nyinyi ni watu ambao mtapewa mtihani wa mambo ya furaha na maudhiko na mema na maovu.
An-Naml 27:47
Inapakia kisomo…
0:00