يَسۡتَخۡفُونَ مِنَ ٱلنَّاسِ وَلَا يَسۡتَخۡفُونَ مِنَ ٱللَّهِ وَهُوَ مَعَهُمۡ إِذۡ يُبَيِّتُونَ مَا لَا يَرۡضَىٰ مِنَ ٱلۡقَوۡلِۚ وَكَانَ ٱللَّهُ بِمَا يَعۡمَلُونَ مُحِيطًا ١٠٨
An-Nisa' 4:108
سورة النساء
Madina
Aya: 108/176
Ukurasa 96
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Wanataka kujificha kwa watu, wala hawataki kujificha kwa Mwenyezi Mungu, naye yu pamoja nao pale wanapo panga njama usiku kwa maneno asiyo yapenda. Na Mwenyezi Mungu anayajua vyema wanayo yatenda. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Wao wanajificha na watu ili wasipate kuyaona matendo yao mabaya, wala hawajifichi na Mwenyezi Mungu Aliyetukuka wala hawamuonei haya, ilhali Yeye, Mtukufu wa mambo, Yupo na wao kwa ujuzi Wake, Anawaona wanapopanga, kipindi cha usiku, maneno Asiyoridhika nayo. Na Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Ameyazunguka(kwa ujuzi Kwake) maneno yao yote na vitendo vyao vyote, hakuna kitu chochote chenye kufichika Kwake.
An-Nisa' 4:108
Inapakia kisomo…
0:00