هَٰٓأَنتُمۡ هَٰٓؤُلَآءِ جَٰدَلۡتُمۡ عَنۡهُمۡ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا فَمَن يُجَٰدِلُ ٱللَّهَ عَنۡهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ أَم مَّن يَكُونُ عَلَيۡهِمۡ وَكِيلࣰا ١٠٩
An-Nisa' 4:109
سورة النساء
Madina
Aya: 109/176
Ukurasa 96
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Hivyo nyinyi mmewatetea hawa katika uhai huu wa duniani. Basi nani atakaye watetea kwa Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama? Au ni nani atakuwa wakili wao wa kumtegemea? -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Haya nyinyi, enyi Waumini, mnatoa hoja za kuwatetea hawa mahaini wa nafsi zao katika huu uhai wa kilimwengu. Basi, ni nani mwenyemuhoji Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kwa kuwatetea wao Siku ya kufufuliwa na kuhesabiwa? Au ni nani atakayekuwa wakili wao Siku ya Kiyama?
An-Nisa' 4:109
Inapakia kisomo…
0:00