إِن تُبۡدُواْ خَيۡرًا أَوۡ تُخۡفُوهُ أَوۡ تَعۡفُواْ عَن سُوٓءࣲ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَفُوࣰّا قَدِيرًا ١٤٩
An-Nisa' 4:149
سورة النساء
Madina
Aya: 149/176
Ukurasa 102
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Mkidhihirisha wema au mkiuficha, au mkiyasamehe maovu, hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira na Muweza. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Amehimiza Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kwamba watu wasamehe, na Akaweka msingi wa jambo hilo kwa kuwa Muumini, ima aidhihirishe kheri au aifiche. Na vilevile katika kukosewa, ima adhihirishe kuwa amekosewa katika hali ya kutafuta haki yake kwa aliyemkosea au asamehe na apuuze. Na kusamehe ni bora. Kwani miongoni mwa sifa za Mwenyezi Mungu ni kuwasamehe waja Wake pamoja na uwezo Wake juu yao.
An-Nisa' 4:149
Inapakia kisomo…
0:00