يَوۡمَئِذࣲ يَوَدُّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَعَصَوُاْ ٱلرَّسُولَ لَوۡ تُسَوَّىٰ بِهِمُ ٱلۡأَرۡضُ وَلَا يَكۡتُمُونَ ٱللَّهَ حَدِيثࣰا ٤٢
An-Nisa' 4:42
سورة النساء
Madina
Aya: 42/176
Ukurasa 85
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Siku hiyo walio kufuru na wakamuasi Mtume watatamani ardhi isawazishwe juu yao. Wala hawataweza kumficha Mwenyezi Mungu neno lolote. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Siku litakapokuwa hilo, watatamani, wale waliomkanusha Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na wakampinga Mtume wasimtii, lau Mwenyezi Mungu Angaliwafanya sawasawa, wao na ardhi, wakawa mchanga ili wasifufuliwe. Na wao hawawezi kumficha Mwenyezi Mungu chochote kilichoko ndani ya nafsi zao, kwa kuwa Mwenyezi Mungu Atakuwa Amefunga midomo yao na kutolewa ushahidi juu yao na viungo vyao wenyewe kwa yale waliokuwa wakiyafanya.
An-Nisa' 4:42
Inapakia kisomo…
0:00