وَيَقُولُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَسۡتَ مُرۡسَلࣰاۚ قُلۡ كَفَىٰ بِٱللَّهِ شَهِيدَۢا بَيۡنِي وَبَيۡنَكُمۡ وَمَنۡ عِندَهُۥ عِلۡمُ ٱلۡكِتَٰبِ ٤٣
Ar-Ra'd 13:43
سورة الرعد
Madina
Aya: 43/43
Ukurasa 255
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na walio kufuru wanasema: Wewe hukutumwa. Sema: Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi baina yangu na nyinyi, na pia yule mwenye ilimu ya Kitabu. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Na wenye kumkanusha Nabii wa Mwenyezi Mungu wanasema, «Ewe Muhammad, hukutumilizwa na Mwenyezi Mungu.» Waambie, «Inatosha kuwa Mwenyezi Mungu ni shahidi juu ya ukweli wangu na urongo wenu, na unatosha ushahidi wa wenye ujuzi wa Kitabu miongoni mwa Mayahudi na Wanaswara kati ya wale waliouamini utume wangu na kwamba yale niliokuja nayo yanatoka kwa Mwenyezi Mungu na akaufuata ukweli na akatoa ushahidi huo waziwazi na asiufiche.
Ar-Ra'd 13:43
Inapakia kisomo…
0:00