وَجَزَٰٓؤُاْ سَيِّئَةࣲ سَيِّئَةࣱ مِّثۡلُهَاۖ فَمَنۡ عَفَا وَأَصۡلَحَ فَأَجۡرُهُۥ عَلَى ٱللَّهِۚ إِنَّهُۥ لَا يُحِبُّ ٱلظَّٰلِمِينَ ٤٠
Ash-Shura 42:40
سورة الشورى
Makka
Aya: 40/53
Ukurasa 487
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na malipo ya uovu ni uovu mfano wa huo. Lakini mwenye kusamehe, na akasuluhisha, basi huyo malipo yake yapo kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye hawapendi wenye kudhulumu. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Na malipo ya ubaya wa mtu mbaya ni kumtesa kwa ubaya mfano wake bila kuzidisha. Na mwenye kumsamehe aliyemfanyia ubaya asimtese, na akatengeneza mapenzi baina yake yeye na yule aliyemsamehe kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu, basi malipo mema ya kusamehe kwake yako kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu Hawapendi wenye kudhulumu wanaowaanza watu kwa uadui na kuwafanyia ubaya.
Ash-Shura 42:40
Inapakia kisomo…
0:00