وَءَاخَرُونَ مُرۡجَوۡنَ لِأَمۡرِ ٱللَّهِ إِمَّا يُعَذِّبُهُمۡ وَإِمَّا يَتُوبُ عَلَيۡهِمۡۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمࣱ ١٠٦
At-Taubah 9:106
سورة التوبة
Madina
Aya: 106/129
Ukurasa 203
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na wapo wengine wanangojea amri ya Mwenyezi Mungu - ama atawaadhibu au atawasamehe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye hikima. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Na miongoni mwa hawa waliojikalisha nyuma wakaacha kuwafuata, enyi Waumini, katika vita vya Tabūk kuna wengine walioahirishwa, ili Mwenyezi Mungu Aaamue juu yao uamuzi Atakaoutoa: ima Awaadhibu Mwenyezi Mungu au Awasamehe. Hawa ni wale waliojuta kwa yale ambayo walifanya. Nao ni Murarah mwana wa al-Rabī‘, Ka‘b mwana wa Mālik na Hilāl mwana wa Umayyaha. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa Anayestahili mateso au msamaha. Ni Mwingi wa hekima katika maneno Yake yote na vitendo Vyake.
At-Taubah 9:106
Inapakia kisomo…
0:00