وَلَا يُنفِقُونَ نَفَقَةࣰ صَغِيرَةࣰ وَلَا كَبِيرَةࣰ وَلَا يَقۡطَعُونَ وَادِيًا إِلَّا كُتِبَ لَهُمۡ لِيَجۡزِيَهُمُ ٱللَّهُ أَحۡسَنَ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ ١٢١
At-Taubah 9:121
سورة التوبة
Madina
Aya: 121/129
Ukurasa 206
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Wala hawatoi cha kutoa kidogo wala kikubwa, wala hawalivuki bonde, ila huandikiwa, ili Mwenyezi Mungu awalipe bora ya waliyo kuwa wakiya- tenda. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Na wala hawatoi matumizi, madogo au makubwa, katika njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawayapiti mabonde katika kutembea kwao pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, katika kupigana kwake jihadi, isipokuwa wataandikiwa thawabu ya tendo lao, ili Mwenyezi Mungu Awalipe mazuri zaidi ya wao kulipwa kwa matendo yao mema.
At-Taubah 9:121
Inapakia kisomo…
0:00