يُولِجُ ٱلَّيۡلَ فِي ٱلنَّهَارِ وَيُولِجُ ٱلنَّهَارَ فِي ٱلَّيۡلِ وَسَخَّرَ ٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَۖ كُلࣱّ يَجۡرِي لِأَجَلࣲ مُّسَمࣰّىۚ ذَٰلِكُمُ ٱللَّهُ رَبُّكُمۡ لَهُ ٱلۡمُلۡكُۚ وَٱلَّذِينَ تَدۡعُونَ مِن دُونِهِۦ مَا يَمۡلِكُونَ مِن قِطۡمِيرٍ ١٣
Fatir 35:13
سورة فاطر
Makka
Aya: 13/45
Ukurasa 436
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Anauingiza usiku katika mchana, na anauingiza mchana katika usiku. Na amelifanya jua na mwezi kutumikia. Kila kimojapo kinakwenda kwa muda maalumu. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu Mlezi. Ufalme ni wake. Na hao mnao waomba badala yake hawamiliki hata ugozi wa kokwa ya tende. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Na Mwenyezi Mungu Anazitia nyakati za usiku ndani mchana, hivyo basi mchana ukarefuka kwa kadiri ya usiku uliopungua; na Anazitia nyakati za mchana ndani ya usiku, hivyo basi usiku ukarefuka kwa kadiri ya mchana uliopungua. Na Amedhalilisha jua na mwezi vikawa vinatembea kwa wakati maaalumu. Huyo aliyefanya hili ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu. Ni Wake Yeye ufalme wote. Na wale mnaowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu hawamiliki hata utandu mwembamba unaozunguka koko ya tende.
Fatir 35:13
Inapakia kisomo…
0:00