وَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّنِ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًاۚ أُوْلَٰٓئِكَ يُعۡرَضُونَ عَلَىٰ رَبِّهِمۡ وَيَقُولُ ٱلۡأَشۡهَٰدُ هَٰٓؤُلَآءِ ٱلَّذِينَ كَذَبُواْ عَلَىٰ رَبِّهِمۡۚ أَلَا لَعۡنَةُ ٱللَّهِ عَلَى ٱلظَّٰلِمِينَ ١٨
Hood 11:18
سورة هود
Makka
Aya: 18/123
Ukurasa 223
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na nani aliye dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye mzulia Mwenyezi Mungu uwongo? Hao watahudhurishwa mbele ya Mola wao Mlezi, na mashahidi watasema: Hawa ndio walio mtungia uwongo Mola wao Mlezi. Laana ya Mwenyezi Mungu iwapate walio dhulumu, -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Na hakuna yoyote aliye dhalimu zaidi kuliko yule aliyemzulia Mwenyezi Mungu urongo. Hao wataorodheshwa kwa Mola wao Siku ya Kiyama, ili Awahesabu kwa matendo yao. Na watasema waliohudhuria miongoni mwa Malaika na Manabii na wengineo, «Hawa ndio wale waliosema urongo kumsingizia Mola wao ulimwenguni. Mwenyezi Mungu Amewakasirikia wao na Amewalaani laana isiyokatika, kwa kuwa udhalimu walioufanya umekuwa ni sifa inayoambatana na wao.
Hood 11:18
Inapakia kisomo…
0:00