۞ مَثَلُ ٱلۡفَرِيقَيۡنِ كَٱلۡأَعۡمَىٰ وَٱلۡأَصَمِّ وَٱلۡبَصِيرِ وَٱلسَّمِيعِۚ هَلۡ يَسۡتَوِيَانِ مَثَلًاۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ ٢٤
Hood 11:24
سورة هود
Makka
Aya: 24/123
Ukurasa 224
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Mfano wa makundi mawili ni kama kipofu kiziwi, na mwenye kuona na anasikia. Je, wawili hawa wanakuwa sawa kwa kufananishwa? Basi, je, hamfikiri? -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Mfano wa makundi mawili, ya ukafiri na Imani, ni mfano wa kipofu asiyeona na kiziwi asiyesikia na yule anayeona na kusikia: kundi la ukafiri haliioni haki likapata kuifuata wala halimsikii mlinganizi wa Mwenyezi Mungu likapata kuongoka kwa sababu yake. Ama kundi la Imani limishaziona hoja za Mwenyezi Mungu na limemsikia mlinganizi wa Mwenyezi Mungu na limemuitikia. Je, yanafanana makundi mawili haya? Kwani hamzingatii na mkafikiri?
Hood 11:24
Inapakia kisomo…
0:00