وَٱصۡنَعِ ٱلۡفُلۡكَ بِأَعۡيُنِنَا وَوَحۡيِنَا وَلَا تُخَٰطِبۡنِي فِي ٱلَّذِينَ ظَلَمُوٓاْ إِنَّهُم مُّغۡرَقُونَ ٣٧
Hood 11:37
سورة هود
Makka
Aya: 37/123
Ukurasa 225
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na unda jahazi mbele ya macho yetu na kwa mujibu wa ufunuo wetu. Wala usinisemeze kuwatetea walio dhulumu. Kwani hao bila ya shaka watazamishwa. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
«Na utengeneze jahazi kwa maangalizi yetu na kwa amri yetu na msaada wetu, hali ya kuwa wewe uko kwenye utunzi wetu na hifadhi yetu, na usitake kwangu kuwapa muhula hawa waliojidhulumu nafsi zao, miongoni mwa watu wako, kwa ukafiri wao, kwani wao ni wenye kuzamishwa kwa mafuriko.» Katika hii aya pana kuthibitisha sifa ya 'ayn (jicho ) kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kwa namna inavyonasibiana na Yeye, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake.
Hood 11:37
Inapakia kisomo…
0:00