رَّبَّنَآ إِنِّيٓ أَسۡكَنتُ مِن ذُرِّيَّتِي بِوَادٍ غَيۡرِ ذِي زَرۡعٍ عِندَ بَيۡتِكَ ٱلۡمُحَرَّمِ رَبَّنَا لِيُقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ فَٱجۡعَلۡ أَفۡـِٔدَةࣰ مِّنَ ٱلنَّاسِ تَهۡوِيٓ إِلَيۡهِمۡ وَٱرۡزُقۡهُم مِّنَ ٱلثَّمَرَٰتِ لَعَلَّهُمۡ يَشۡكُرُونَ ٣٧
Ibrahim 14:37
سورة إبراهيم
Makka
Aya: 37/52
Ukurasa 260
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Mola wetu Mlezi! Hakika mimi nimewaweka baadhi ya dhuriya zangu katika bonde lisilo kuwa na mimea, kwenye Nyumba yako Takatifu, ewe Mola wetu Mlezi, ili washike Sala. Basi zijaalie nyoyo za watu zielekee kwao, na waruzuku matunda, ili wapata kushukuru. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
«Ewe Mola wetu! Mimi nimewafanya watoto wangu wakae kwenye bonde lisilo na mimea wala maji, penye ujirani na mji wako mtakatifu. Mola wetu! Mimi nimefanya hilo kwa amri Yako, ili wasimamishe Swala kwa namna yake itakikanayo, basi ifanye myoyo ya baadhi ya viumbe vyako ilemee kwao na ipendelee, na uwape riziki ya kila aina ya matunda wakiwa mahali hapa, ili wakushukuru kwa neema zako.» Mwenyezi Mungu Akakubali maombe yake.
Ibrahim 14:37
Inapakia kisomo…
0:00