وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا مُوسَىٰ بِـَٔايَٰتِنَآ أَنۡ أَخۡرِجۡ قَوۡمَكَ مِنَ ٱلظُّلُمَٰتِ إِلَى ٱلنُّورِ وَذَكِّرۡهُم بِأَيَّىٰمِ ٱللَّهِۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتࣲ لِّكُلِّ صَبَّارࣲ شَكُورࣲ ٥
Ibrahim 14:5
سورة إبراهيم
Makka
Aya: 5/52
Ukurasa 255
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na tulimtuma Musa pamoja na miujiza yetu, tukamwambia: Watoe watu wako kwenye giza uwapeleke kwenye mwangaza. Na uwakumbushe siku za Mwenyezi Mungu. Hakika katika hayo zipo ishara kwa kila mwenye kusubiri akashukuru. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Na kwa hakika tulimtuma Mūsā kwa Wana wa Isrāīl na tukamsaidia kwa miujiza yenye kuonyesha ukweli wake na tukammpa amri awalinganie wao kwenye Imani, ili awatoe wao kutoka kwenye upotevu awatie kwenye uongofu na awakumbushe neema za Mwenyezi Mungu na mateso Yake katika wakati wake. Katika kukumbusha huku mambo hayo kuna dalili nyingi kwa kila mvumilivu sana juu ya utiifu wa Mwenyezi Mungu, kuyaepuka yaliyoharamishwa na Yeye na kuyakubali maandiko Yake, mwenye kushukuru sana, mwenye kusimama kutekeleza haki za Mwenyezi Mungu na anayemshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema Zake. Aina mbili hizi za watu zimetajwa mahsusi, kwa kuwa wao ndio wanaozingatia hizo dalili na hawaghafiliki nazo.
Ibrahim 14:5
Inapakia kisomo…
0:00