فَأَعۡرَضُواْ فَأَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِمۡ سَيۡلَ ٱلۡعَرِمِ وَبَدَّلۡنَٰهُم بِجَنَّتَيۡهِمۡ جَنَّتَيۡنِ ذَوَاتَيۡ أُكُلٍ خَمۡطࣲ وَأَثۡلࣲ وَشَيۡءࣲ مِّن سِدۡرࣲ قَلِيلࣲ ١٦
Saba' 34:16
سورة سبأ
Makka
Aya: 16/54
Ukurasa 430
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Lakini wakaacha. Tukawapelekea mafuriko makubwa, na tukawabadilishia badala ya bustani zao hizo kwa bustani nyengine zenye matunda makali machungu, na mivinje, na kidogo katika miti ya kunazi. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Wakaipa mgongo amri ya Mwenyezi Mungu, wakaacha kumshukuru na wakawakanusha Mitume, tukawatumia mafuriko yenye kubomoa yaliyo na nguvu, yaliyoliharibu bwawa la maji na yakayazamisha mabustani. Na tukawageuzia mabustani yao mawili yenye kutoa matunda yakawa ni mabustani mawili yenye miti michache ya khamṭ, nayo ni miti ya matunda machungu yenye ladha ya kuchukiza, na athl, nayo ni miti inayofanana na ṭarfā ’isiyokuwa na matunda, na mikunazi michache yenye miba mingi.
Saba' 34:16
Inapakia kisomo…
0:00