إِنَّ ٱلَّذِينَ لَا يَرۡجُونَ لِقَآءَنَا وَرَضُواْ بِٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَٱطۡمَأَنُّواْ بِهَا وَٱلَّذِينَ هُمۡ عَنۡ ءَايَٰتِنَا غَٰفِلُونَ ٧
Yunus 10:7
سورة يونس
Makka
Aya: 7/109
Ukurasa 209
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Hakika wasio taraji kukutana nasi, na wakaridhia maisha ya dunia na wakatua nayo, na walio ghafilika na Ishara zetu, -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Hakika ya wale ambao hawana matumaini ya kukutana na sisi Akhera kwa kuhesabiwa na yanayofuatia ya malipo juu ya matendo kwa kuwa wanakanusha kufufuliwa, wakaridhika na maisha ya ulimwenguni kuwa ni badala ya Akhera, wakajitegemeza nao huo ulimwengu, na wale ambao wao ni wenye kughafilika na alama zetu zilizoko ulimwenguni na zilizomo kwenye Sheria.
Yunus 10:7
Inapakia kisomo…
0:00